EXHIBITS

Mradi wa Usambara: Mandhari ya Mabadiliko na Endalevu katika Milima Usambara ya Mashariki, c. 1910

Summary

Banner for Usambara Digital ExhibitKaribu kwenye Maonyesho ya kimtandao ya Mradi wa Historia ya jamii ya watu wa Usambara. Maonyesho hayayana picha za mwanzo za karne ya ishirini kutoka kwa Walther Dobbertin, mpiga picha mtaalamu mkazi wa Afrika Mashariki waUjerumani kuanzia 1903 hadi 1914. Mbali na picha za Dobbertin, timu ya Mradi wa Usambara iligundua na kupiga picha kadhaa ya mandhariya awali mwaka wa 2016 na 2019.

Mbali na pichazao za maisha ya Wajerumani katika Afrikaya Mashariki, pichaza maonyesho haya zinaonyesha juhudi zaWaafrika wanaotekeleza mradi wa kurejesha ikolojia kwa kutumia mbinu zilizojaribiwa kwa muda ambazo zilihifadhi udongo na kutegemea aina mbalimbali za mimea ya kigeni na ya kiasil.

Mradi Mkubwa Zaidi

Maonyesho haya ni sehemu ya Mradi wa Historia ya Mandhari ya Usambara, unaolenga kuandika historia ya mabadiliko ya mandhari katika Milima ya Usambara Kaskazini-Mashariki mwa Tanzania. Walioshirikiana nao ni pamoja na Baraza la Wazee wa Mlalo, Baraza la Wazee wa Usambara, Ofisi ya Maktaba ya Chuo Kikuu cha Utah State of Digital Initiatives, Idara ya Maktaba Maalum na Nyaraka za Chuo Kikuu cha Utah State, Kivatiro Hamza Kitojo, Sufian Shekoloa (marehemu) na Chris Conte, Profesa, Chuo Kikuu cha Jimbo la Utah 

Kazi hadi kufikia sasa

  • 2016 – Kikundi  cha mradi  kilipata maeneo ya mandhari ya Dobbertin na kufanya mahojiano ya awali ili kubaini uwezekano wa mradi huo.
  • 2019 Kikundi cha mradi kilifanya vipindi vya usaili vya vikundi huko Mlalo, Gare, Kwefingo, na Vuga katika mwezi wa Julai. 

Kazi Ifuatayo

  • 2022 - Kukamilisha na kuonyeshe maonyesho ya mikutano. 
  • 2022 - Kukamilisha marudio ya kwanza ya maonyesho ya kimtandao. 
  • 2022 - Hadithi  na simulizi za Kilimo mseto, uchoraji wa ramani, na orodha. 
  • 2022 - Kutambua miradi mipya na washiriki wapya wa timu.