EXHIBITS

English

Mazingira ya Milima ya Usambara

Historia ya Asili

Milima ya Usambara ni sehemu ya Milima ya Tao la Mashariki, ambayo inaanzia kusini mwa Kenya hadi kusini mwa Tanzania. Miinuko ni ya zamani, tukizungumza kijiolojia. Iliundwa  takribani miaka milioni mia moja iliyopita ikitengeneza milima na mambonde kwenye mstari wa zamani wa  mabonde. Milima hiyo inainuka  juu ya tambarare zinazozunguka na kama safu za pwani na hupata mvua za monsuni zinazonyesha katika Bahari ya Hindi. Mvua thabiti za msimu, hata wakati wa kipindi cha mamilioni ya miaka ya miamba[Pleistocene], ilikuza ukuaji wa misitu ya Uwoto wa asili {tropical}katika Mikoa ya Mashariki. Mwinuko  na viwango vya joto pia vilikuza anuwai ya viumbe hai{kibaolojia} kwa kipindi kifupi sana, hivyo kwamba taasisi ya kisayansi inachukulia misitu ya milima kuwa maeneo yenye anuwai ya kibaolojia ya ulimwengu na maadili ya juu ya uhifadhi.