EXHIBITS

English

Shamba la Kwai

(4°44'6.36"S, mwinuko mita 1650 asl)

Utangulizi

Kwai iko maili chache tu kutoka Gare, lakini ipo kwenye mwinuko wa mita 1600 asl, bonde la Kwai limekaa juu ya eneo la kilimo lenye joto na mvua za Usambara chini ya mita 1400. Kwa karne nyingi kabla ya Wajerumani walichukua bonde hilo mwaka wa 1896, Kwai ilitumika kama eneo la kutegemewa na Wambugu la kufuga mifugo ya ng'ombe na mbuzi. Kwai ilikuwa na maana muhimu kama eneo la vita wakati wa magonjwa ya ng'ombe ya miaka ya 1890. Kulingana na hadithi zilizosimuliwa huko Kwai, huo ulikuwa wakati ambapo wapiganaji wa Kimasai kutoka nyanda za chini waliingia milimani wakiwa na nia ya kuiba mifugo. Mlango wa bonde kutoka chini ni mwembamba sana, karibu umefichwa, na kwa hivyo unaweza kutetewa. Damu ya wa Mbugu ilimemwagika pale na hivyo ikawa mahali pa heshima.

Wakati habari za uwezekano  wa kilimo wa  eneo la bonde la  Kwai zilipoenea kwa serikali ya Ujerumani, tume ya ardhi ya kikoloni iliteka zaidi ya hekta elfu moja, ambazo zilizunguka sehemu kubwa ya bonde na ardhi yenye  wastani wa mtremko wa ardhi  kila upande inavyoonekana kwenye picha.

DNO-0163_Bild105-DOA6388.jpg

Emil Eick, mwenyewe mmiliki- na msimamizi wa shamba kubwa huko mashariki mwa Ujerumani, alihudumu kama meneja wa Kwai kuanzia 1896 hadi 1902. Alisimamia uwekaji wa vitalu vya miti, na upandaji wa bustani juu ya makazi bado ulionekana katika miaka ya 1910. Mnamo 1902, serikali ya Ujerumani ya Afrika Mashariki ilitangaza kushindwa katika shamba la majaribio na Eick aliondoka mwaka wa 1903. Kisha serikali ilikodisha kwa Ludwig Illich, ambaye wakati huo alikuwa meneja wa shamba la Ubiri (karibu na Lushoto).  Illich aliendesha na kusimamia shamba la ng'ombe ambalo Dobbertin alipiga picha zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Wakati serikali ya Uingereza ilipochukua umiliki wa koloni hilo baada ya Vita vya Kwanza vya Kidunia, ofisi ya kikoloni ya Mlinzi wa Mali ya Adui ilikodisha shamba hilo kwa mpishi mstaafu wa jeshi la wanamaji aitwaye Woodcock, ambaye alipatwa na hali ya wasiwasi. Mauaji yake (kupitia   ukurasa wa gazeti la Tanzania Standard, Woodcock aliuwawa na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mauwaji hayo.) mnamo 1953, yalichochea wamiliki wapya wa kukodisha na kufungua bonde kwa matumizi ya ardhi ya ndani. Muda mfupi baadaye, watu walibomoa kabisa majengo ya shamba hilo, kwa kutumia vifaa katika miradi ya ujenzi wa jamii. Kwa hivyo wakulima walifutilia mbali masalia yoyote ya asili ya ukoloni.